• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasikitishwa na vyombo vya habari vya magharibi kuwa na upendeleo katika kuripoti suala la Xinjiang

  (GMT+08:00) 2019-12-09 19:29:09

  China imeeleza kusikitishwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi vinavyofuatilia kwa karibu suala la Xinjiang kukaa kimya kwa pamoja baada ya Televisheni ya CGTN ya China hivi karibuni kutangaza filamu mbili fupi kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi mkoani humo.

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema vyombo vya habari vina wajibu kwa jamii na vinapaswa kueleza ukweli kwa watazamaji, badala ya kupanga msimamo kabla ya kuripoti na kuwa na upendeleo katika kuripoti na kuwaelezea vibaya watazamaji hao.

  Hua alikuwa na maswali kwa wanahabari wa nchi za magharibi walioshiriki mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika hii leo, akisema,

  "Mnafuatilia sana habari zinazoenezwa na waongo kuhusu suala la Xinjiang, lakini mnakataa kuripoti ukweli na picha halisi kuhusu Xinjiang. Je, kwa nini? Mna wasiwasi gani? Mnaogopa nini? Mbona hamtaki kukaa chini na kutafakari kwa makini?"

  Filamu hizo mbili zimetumia ushahidi mwingi kueleza juhudi na kujitolea kwa China katika vita dhidi ya ugaidi na kuonesha jinsi Vuguvugu la Kiislamu la Mashariki ya Turkestan, ETIM linavyoeneza msimamo mkali, kuchochea chuki za kikabila, kuwadhalilisha wanawake na watoto na kufanya mashambulizi ya kigaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako