• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakazi wa Xinjiang wailaani Marekani kwa kupitisha mswada kuhusu mkoa huo

  (GMT+08:00) 2019-12-09 19:38:05

  Hivi karibuni, Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani lilipitisha "mswada wa mwaka 2019 wa sera ya haki za binadamu za Wauyghur". Kitendo hiki kimelaumiwa na wakazi wa mkoani Xinjiang, ambao wamesema hakuna nguvu yoyote inayoweza kuzuia maendeleo ya mkoa huo, na usumbufu na hila yoyote vitazidi kuongeza mshikamano wa watu milioni 25 wa mkoa huo.

  Mwenyekiti wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang Bw. Shocklaty Zacher amesema, muswada huo umekiuka kanuni ya kimsingi ya sheria na uhusiano wa kimataifa kwa kuingilia kati mambo ya ndani ya China. Ameihimiza Marekani iache ubaguzi wa kisiasa, na kutoweka vigezo tofauti katika juhudi za kupambana na ugaidi na kuondoa msimamo mkali.

  Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanawake la mkoa wa Xinjiang Bibi Ainur Mahsati ameeleza kusikitishwa na Marekani kwa kupaka matope sera zinazotekelezwa na serikali ya China mkoani humo. Anasema,

  "Watu wa makabila mbalimbali mkoani Xinjiang wanafahamu vizuri kuwa, bila ya Chama cha Kikomunisti cha China, hawawezi kupata masikilizano, utulivu na maisha bora. Hatua mbalimbali za kudumisha utulivu zinazotekelezwa mkoani Xinjiang zinapongezwa na watu, na zinalinda haki zao za binadamu. Hatutaruhusu nguvu yoyote ya nje kuingilia kati mambo ya Xinjiang."

  Bibi Gulichire Aireti kutoka kabila la Wauyghur ni mtoto wa aliyekuwa naibu mkuu wa polisi ya wilaya ya Pishan. Mwezi Septemba mwaka 2016, baba yake huyo aliuawa katika msako dhidi ya magaidi. Bibi Aireti anasema,

  "Marekani haina haki ya kunyoshea vidole maisha yetu. Utulivu wa mkoa wa Xinjiang umepatikana kutokana na juhudi za mashujaa akiwemo baba yangu. Siruhusu mtu yeyote kupaka matope mkoa wetu mzuri."

  Kuhusu vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi vinavyowasaidia vijana kuondokana na ugaidi na msimamo mkali mkoani Xinjian, mwenyekiti wa serikali ya mkoa huo Bw. Shokhart Zakir amesema, kutokana na msaada wa serikali, wahitimu wa vyuo hivyo wamepata ajira za uhakika, wameboresha maisha yao na wamekuwa na maisha mazuri nay a furaha. Amesema ripoti za vyombo vya habari vya kigeni vinavyodai kuwa kuna wanafunzi zaidi ya milioni moja kwenye vyuo hivyo sio za kweli, kwani idadi ya wanafunzi inabadilika kila mara, kwa kuwa kuna wanafunzi wanaohitimu na wanaojiandikisha mara kwa mara.

  Bw. Abulati Atir kutoka mji wa Hetian mkoani Xinjiang ni mhitimi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Hetian, mkoani humo, na aliwahi kuathiriwa na msimamo mkali wa kidini. Akiwa chuoni hapo, alijifunza lugha sanifu ya Kichina, mambo ya sheria na ustadi wa kazi, na sasa amepata kazi nzuri kwa msaada wa serikali. Anasema,

  "Mswada uliopitishwa na Marekani ni upuuzi tu, na hatuwezi kukaa kimya kuhusu kauli hiyo ya kufarakanisha Xinjiang. Kituo cha mafunzo ya ufundi stadi kilibadilisha maisha yangu, na mimi na familia yangu tunaridhika sana na maisha ya hivi sasa."

  Hivi karibuni, Shirika kuu la Utangazaji la China lilitoa filamu mbili za kumbukumbu kuhusu mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mkoani Xinjiang, China, mashambulizi ambayo yamedhuru vibaya haki za binadamu za watu wa makabila mbalimbali mkoani humo. Filamu hizo zimefuatiliwa sana na watu, ila zimepuuzwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi. Hali hii inaonesha vigezo tofauti za nchi hizo kuhusu ugaidi, na kutoa ishara ya hatari kwa makundi ya kimataifa ya kigaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako