• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuendelea kutoa mazingira mazuri ya kibiashara kwa wawekeaji wa nchi za nje

  (GMT+08:00) 2019-12-09 20:39:00

  Msaidizi wa waziri wa biashara wa China Bw. Ren Hongbin leo hapa Beijing amesema, China inazingatia kuboresha mazingira ya kibiashara, kuzidisha mageuzi, na kuongeza uhai wa sera na uwezo usiodhihirika wa uvumbuzi, ili kuendelea kutoa mazingira mazuri ya kibiashara na uhakikisho wa sera kwa maendeleo ya makampuni ya wawekeaji wa nchi za nje.

  Pia amesema, ili kutimiza hilo, China itaendelea kutafuta mfumo mpya wa usimamizi na mfumo wa sera, na kuhimiza wawekeaji wa nchi za nje kuwekeza katika sekta zinazositawi, na kuongeza kuwa, biashara kati ya China na nchi za nje kwa mwaka huu ilikua kwa utulivu.

  Takwimu mpya zilizotolewa na serikali ya China zimeonesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi Novemba, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje ilifikia dola trilioni 3.67, ambayo iliongezeka kwa asilimia 2.4, na inakadiriwa kuwa thamani ya ujumla ya biashara kwa mwaka mzima itafikia karibu dola za kimarekani trilioni 4.27.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako