• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bruno asema siri ya kumtwanga Nathaniel May raia wa Australia ni kujituma bila kukata tamaa

  (GMT+08:00) 2019-12-10 08:46:38

  Bruno Tarimo maarufu kama 'Vifuaviwili' bondia wa ngumi za kulipwa amesema kuwa siri kubwa ya kupata ushindi mbele ya bondia Nathaniel May raia wa Australia ni kujituma bila kukata tamaa. Pambano hilo la raundi 10 la uzito wa kg 59 lililofanyika Ijumaa nchini Sydney lilikuwa ni la kuwania mkanda wa International Super Featherweight Defense (IBF) ambao ameutwaa Vifuaviwili baada ya kushinda kwa pointi. Vifuaviwili alisema kuwa alijipanga kupeperusha bendera ya Tanzania akiwa ugenini jambo ambalo lilifanikiwa kujibu kwa kupata ushindi. Vifuaviwili ameweka rekodi nzuri kwa Tanzania kwa upande wa ngumi kimataifa akicheza jumla ya mapambano 28 amepoteza pambano moja kwa pointi na akishinda jumla ya mapambano 27.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako