• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha ulinzi cha China mkoani Macao chalinda utulivu na usalama wa mkoa huo

    (GMT+08:00) 2019-12-10 17:59:09

    Huu ni mwaka wa 20 tangu Macao kurudi China. Katika miaka hiyo, kikosi cha ulinzi cha China kwenye mkoa huo wenye utawala maalumu kimefuata kithabiti sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" na sheria husika, na kutekeleza majukumu ya kulinda mamlaka ya taifa, utulivu na ustawi wa Macao.

    "Natii taifa langu na wananchi wangu!"

    Ni saa nne asubuhi, kwenye kituo cha kikosi cha ulinzi cha China mkoani Macao, kikundi cha askari maalumu walikuwa wakifanya mazoezi. Kwa mujibu wa sheria ya kikosi cha ulinzi cha China mkoani Macao, majukumu ya kikosi hicho ni pamoja na kujibu na kuzuia uvamizi, kulinda usalama wa mkoa huo, na kufanya uokoaji.

    Mwaka 1999, wakati kikosi hicho kilipoanza kazi mkoani Macao, hakikuwa hata na kituo cha kudumu. Kilikaa kwenye jengo moja la ghorofa, na kufanya mazoezi ndani ya jengo hilo. Sasa kikosi hicho kina miundombinu bora ikiwemo kiwanja na eneo la kufanya mazoezi, madarasa ya kujifunza, bwawa la kuogelea, na vyumba vizuri vya kulala.

    Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, uwezo wa kikosi cha ulinzi cha China mkoani Macao umeimarika siku hadi siku. Kikosi hicho kimefanya luteka 14 mkoani humo, luteka ya pamoja na vikosi vya Malaysia na Thailand, na luteka ya pamoja na kikosi cha Laos. Mkuu wa kikundi cha askari maalumu wa kikosi hicho Li Yangchun anasema,

    "Zamani hatukufanya luteka pamoja na majeshi ya nchi nyingine. Hivyo kabla ya luteka hiyo tulifanya mazoezi kwa mwezi mmoja."

    Mazoezi ya kila siku pia yameongeza mwamko wa askari hao wa kupenda na kulinda Macao. Askari wa kikosi hicho Wen Junlin anasema,

    "Nimekuwa hapa kwa miaka miwili. Watu wa China bara na Macao ni familia moja. Madhumuni yangu ya kujiunga na jeshi ni kulinda taifa letu. Katika miaka hiyo nimefanya mazoezi kwa makini, endapo kuna tukio la dharura, sitasita kuwalinda watu wa hapa, hata kutoa maisha yangu."

    Mkuu wa mkoa wa Macao Bw. Cui Shian amesema watu wa Macao na askari hao wamekuwa kitu kimoja. Anasema,

    "Kikosi hicho ni nguvu imara ya kutulinda. Wamacao wanawapenda sana askari hao, kwani wamefanya kazi nyingi kwa ajili yao. Sisi ni kitu kimoja."

    Katika miaka 20 iliyopita, kikosi hicho kimekua na kuwa nguvu yenye ufanisi mkubwa ya kiulinzi, na wametekeleza vizuri majukumu yao, na kupongezwa sana na watu wa mkoa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako