• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ehtiopia: Ethiopia yasaini makubaliano ya ujenzi wa barabara na kampuni za China

    (GMT+08:00) 2019-12-10 18:45:53

    Mamlaka ya Barabara nchini Ethiopia (ERA) imesaini mikataba ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya dola milioni 188.5 za Amerika na kampuni nne za China.

    Katika taarifa kwa waandishi wa habari, ERA imesema mikataba minne hiyo ni ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 299.

    Makubaliano ya kwanza ya ujenzi wa barabara ambayo yalitiwa saini kati ya ERA na Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya Ningxia yanatarajiwa kugharimu dola milioni 45.

    Makubaliano ya pili ni kati ya ERA na China Railway 14 Bureau Group ya dola milioni 58 na ya tatu ni kati ya Hebei Construction Group ya dola milioni 46.

    Serikali ya Ethiopia inafanya miradi mikubwa ya miundombinu ya barabara, inayolenga kuongeza barabara za lami nchini humo kutoka kilomita 100,000 mwaka 2015 hadi kilomita 200,000 mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako