• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Mfuko  wa Ulinzi wa Amana watoa wito kwa raia kusahisha maelezo ya akaunti zao

  (GMT+08:00) 2019-12-10 18:46:12
  Mfuko wa Ulinzi wa Amana kwa umma nchini Uganda unatoa wito kwa raia wote kusahisha maelezo ya akaunti zao za benki ili kuiwezesha hazina hiyo kuhifadhi habari zao katika mfumo wa kompyuta.

  Mfumo huo unatarajiwa kupunguza taratibu za kufanya malipo kwa wanaohifadhi fedha zao ikiwa benki itafungwa.

  Mnamo Desemba 4, Mfuko wa Ulinzi wa Amana ulielezea kwamba mtu yeyote ambaye ana akaunti zaidi ya moja katika benki tofauti anapaswa kusahisha maelezo yote ya akaunti yao kwa ili benki moja ikifungwa, hazina hiyo inaweza kutumia akaunti zao zingine kulipa pesa zao.

  Aidha hazina hiyo inashauri watu kusahisha nambari zao za simu kwenye benki zao kwa sababu pia hazina hiyo itatumia simu kufanya malipo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako