• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viongozi watakiwa kuwapa nafasi zaidi vijana Afrika

  (GMT+08:00) 2019-12-10 18:46:29
  Viongozi wa bara Afrika wamehimizwa kupatia kipaumbele masuala yanayohusu vijana.

  Suala hilo lilijitokeza katika kongamano linaoendelea nchini Rwanda la Kusi Ideas Festival, kuhusiana na masuala ya Bara Afrika katika kipindi cha miaka 60 ijayo.

  Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo (UNCTAD), Dkt Mukhisa Kituyi aliwasisimua waliohudhuria kongamano, akisema kizazi cha sasa kinatilia maanani ushirikiano badala ya mashindano ili kufanikiwa.

  Dkt Kituyi alisema bara hili linafaa kuwaruhusu vijana kutangamana, kuwekeza na kuhamia taifa moja hadi jingine bila kuwekewa vikwazo vya usafiri na kutangamana.

  Marais wa nchi mbalimbali barani pia waliombwa kushirikiana na kufungua mipaka ya mataifa yao kwa raia kutoka nje ili kuwaruhusu kufanya biashara na kuinua uchumi wa nchi husika.

  Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Maendeleo Nchini Rwanda(RDB), Bi Clare Akamanzi alisema mataifa hayafai kuhofia kuondoa vikwazo vya mipaka, akisema uhuru wa kufanya biashara utasaidia kustawisha nchi za Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako