• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawekezaji watakiwa kuwekeza EPZA

    (GMT+08:00) 2019-12-10 18:46:49
    Wawekezaji wa ndani wamehimizwa kutumia fursa zinazotolewa na Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA), kuanzisha viwanda ili kuchangia ukuaji wa uchumi.

    Mpaka sasa asilimia 43 ya viwanda katika Mamlaka ya EPZA vinamilikiwa na wawekezaji wazawa ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na uboreshaji wa mazingira ya biashara na serikali.

    Ofisa Mwandamizi Uhamasishaji wa EPZA, Panduka Yonazi amesema Mamlaka ya EPZA inatoa fursa na huduma mbalimbali kama kuwezesha uwekezaji, kutoa leseni na vivutio mbalimbali ambavyo vitamsaidia mwekezaji mzawa kuwekeza katika viwanda.

    Alisema mamlaka inatoa huduma kwa wawekezaji kabla ya uwekezaji, wakati na baada ya uwekezaji ili kuwapatia taarifa muhimu za namna ya kuwekeza katika maeneo ya ukanda maalum wa kiuchumi ya EPZ na SEZ.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako