• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Uholanzi kufadhili uchukuzi wa majini Rwanda

  (GMT+08:00) 2019-12-10 18:47:13
  Serikali ya Rwanda imepata ufadhili kutoka Uholanzi kufadhili maendeleo ya bandari nne katika Ziwa Kivu, inayotarajiwa kukuza uchukuzi wa majini, biashara na utalii.

  Mpangilio wa ruzuku hiyo ni kwamba Uholanzi itafadhili asilimia 45 ya ujenzi wa bandari na vifaa ambavyo vitaboresha usafiri wa kivuko na mizigo kati ya bandari za Rwanda.

  Rwanda kwa sasa inategemea sana usafiri wa barabarani ambao una gharama kubwa .

  Mradi huo wa franc bilioni 22 utajengwa katika wilaya nne za Rubavu (Nyamyumba), Rusizi (Bugiki), Karongi (katika soko la mpaka wa Karongi), na Rutsiro (mkoa wa Nkora) na utaanza kutumika ifikapo mwaka 2022.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako