• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa ufafanuzi wa kisheria ili kuhakikisha idara za utawala zinatimiza ahadi zao

  (GMT+08:00) 2019-12-10 18:51:18

  Mahakama Kuu ya Watu wa China imetoa ufafanuzi wa kisheria wa kesi zinazohusiana na makubaliano ya kiutawala, ikilenga kulinda vizuri haki za watu na maslahi yao katika kesi zinazohusisha idara za utawala.

  Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Kesi iliyo chini ya Mahakama hiyo, Huang Yongwei amesema, ufafanuzi huo pia unalenga kuhakikisha kuwa idara hizo zinatimiza ahadi zao katika makubaliano yao na wananchi, wanasheria ama taasisi nyingine ili kutimiza malengo ya kiutawala ama huduma za jamii.

  Kutokana na ufafanuzi huo, mahakama nchini China zinapaswa kushughulikia kesi za kiutawala zilizofunguliwa na wananchi, wanasheria ama taasisi nyingine kuhusu kesi za madai zinazohusisha masuala mbalimbali ikiwemo ardhi na nyumba, upangaji au malipo ya nyumba za serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako