• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa serikali ya Hong Kong aahidi kuendelea kufanya juhudi kulinda haki za binadamu na uhuru

    (GMT+08:00) 2019-12-10 19:05:28

    Mkuu wa mkoa wenye utawala maalum wa Hong Kong, China, Carrie Lam amesema serikali yake itaendelea kufanya kila linalowezekana kulinda haki za binadamu na uhuru wa wakazi wa Hong Kong.

    Lam amewaambia wanahabari kuwa, uhuru unalindwa kwa kufuata Sheria ya Kimsingi na Sheria ya Haki za Binadamu ya Hong Kong, na vipengele vya Mkataba wa Kimataifa kuhusu Uraia na Haki za Kisiasa vinavyoihusu Hong Kong pia bado vinatekelezwa.

    wakati huohuo, Polisi walitoa barua ya kuruhusu mkusanyiko wa umma na maandamano yaliyofuata katika kisiwa cha Hong Kong Jumapili. Shughuli hiyo ilifanyika Amani, lakini vitendo vya kimabavu bado viliripotiwa wakati baadhi ya watu walipowasha moto nje ya mahakama mbili za Hong Kong na kuharibu maduka.

    Lam amekosoa vitendo hivyo na kusema serikali yake haitavumilia uharibifu wowote kwa mujibu wa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako