Kinda wa Barcelona Ansu Fati usiku wa Disemba 10 2019 amevunja rekodi iliyodumu kwa miaka 22 ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga goli UEFA Champions League akiwa na umri wa miaka 17 na siku 40. Ansu Fati akitokea benchi dakika ya 85 kuchukua nafasi ya Carles Perez katika mchezo wa Barcelona dhidi ya Inter Milan uliomalizika kwa Barcelona kupata ushindi wa 2-1 alifunga goli la ushindi dakika ya 86 na kuandika rekodi hiyo. Awali rekodi hiyo iliwekwa na Peter Ofori Quaye, Oktoba 1997 akiwa na umri wa miaka 17 na siku 194 akiichezea Rosenborg dhidi ya Olympiacos, hata hivyo Ansu Fati ana rekodi ya kuwa mchezaji wa Barcelona mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga goli na watatu LaLiga kwa wenye umri mdogo kuwahi kufunga goli LaLiga.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |