• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Napoli yamtimua kazini meneja wake Carlo Ancelotti licha ya kuwaongoza kuingia hatua ya mtoano Champions League

  (GMT+08:00) 2019-12-11 08:13:27

  Napoli imemtimua kazini meneja wake Carlo Ancelotti chini ya saa tatu baada ya kuwaongoza kuingia hatua ya mtoano katika Champions League. Klabu hiyo ya Serie A imekuwa ikisuasua na kutoshinda mechi tisa kwenye michuano yote hadi jana ilipofanikiwa kuwabanjua wageni wao Genk kwa magoli 4-0. Ancelotti alikuwa kwenye msimu wake wa pili akiingoza klabu ya Napoli lakini wamekuwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi baada ya kuwa na matokeo mabaya. Mwezi uliopita Ancelotti na wachezaji walikuwa kwenye mzozo mkubwa na rais wa klabu Aurelio de Laurentiis. Rais huyo aliamuru timu iingie kambini kwa wiki nzima lakini meneja huyo na wachezaji wote walirejea nyumbani. Ancelotti, aliyeshinda Premier League na FA Cup Double akiwa na Chelsea mwaka 2009-10, amekuwa akihushishwa kutaka kwenda klabu za Arsenal na Everton.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako