• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WTO yasimamisha idara yake ya kusikiliza kesi

    (GMT+08:00) 2019-12-11 18:29:44

    Mkutano wa 5 wa mwaka huu wa kamati kuu ya Shirika la Biashara Duniani WTO umemalizika katika makao makuu yake yaliyoko Geneva, Uswis.

    Kutokana na kususiwa na Marekani, muswada wa kuboresha idara ya kusikiliza kesi za mashtaka ya Shirika hilo haukupitishwa. Mkurugenzi wa WTO Roberto Azevedo anasema:

    "Nchi wanachama hazikuweza kufikia makubaliano kuhusu muswada wa kuboresha idara ya kusikiliza kesi za mashtaka. Hivyo, idara hiyo haitafanya kazi kuanzia leo. Jambo linalopaswa kusisitizwa ni kwamba, sheria za WTO bado zitaendelea kufanya kazi. Nchi nyingi wanachama zitaendelea kufuata sheria hizo na kulinda maslahi yao ya uchumi. Pia tunatarajia kudumisha uhusiano mzuri na wenzi wa kibiashara."

    Amesema, China na wanachama wanachama wengine zinataka kutafuta utatuzi wa suala hilo kwa haraka, ambao ni muhimu kuchagua njia sahihi na kudumisha majadiliano ya wazi.

    "China ikiwa ni mshiriki kutoka mwanzoni, pamoja na nchi wanachama wengine zinapenda kupata utatuzi unaofaa. Hivi sasa, tunapaswa kujua jinsi ya kuendelea mbele. Jambo la kwanza ni kufanya mazungumzo ya dhati na yenye uwazi ili kupata utatuzi na kuutekeleza. "

    Kwenye mkutano huo, mjumbe wa kudumu wa China katika WTO Bw. Zhang Xiangchen ameilaumu Marekani kwa kuharibu idara ya kusikiliza kesi za mashtaka. Amesema, kusimamishwa kazi kwa idara hiyo ni pigo kubwa kwa mfumo wa pande nyingi wa biashara tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo, na pia itauletea utaratibu wa biashara ya dunia hasara na matokeo mabaya yasiyoweza kukadiriwa.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, katika miaka 25 iliyopita tangu kuanzishwa kwa WTO, idara hiyo ilihukumu zaidi ya kesi 200, na kutoa mchango muhimu kwa utatuzi wa mivutano ya kibiashara. Hivyo inathaminiwa na nchi zinazofuata utaratibu wa pande nyingi, lakini imepuuzwa na nchi chache zinazotekeleza sera ya umwamba katika masuala ya kibiashara. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kutatua changamoto inayokabili idara hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako