• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MAGONGO: USIU-A yaifunza Sailors jinsi ya kucheza magongo

  (GMT+08:00) 2019-12-11 18:32:21

  Matumaini ya Sailors kumaliza ya sita katika jedwali la Ligi Kuu ya magongo ya wanaume nchini Kenya yaliota mbawa ilipolimwa mabao 5-2 na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha USIU-A Uwanjani City Park, Nairobi. USIU-A ya kocha Willis Okeyo ilicheza vizuri licha ya kuwa na upinzani mkali, na kuvuna alama zote kutokana na magoli ya Brian Kiplimo, Richard Wandera, Lawrence Makacha, Chidi Victor na Smith Ngari waliocheka na wavu mara moja kila mmoja. Nao Abraham Musee na Douglas Nyerere kila mmoja aliitingia Sailors goli moja. Matokeo hayo yalifanya USIU-A kumaliza ya sita kwa alama 26, tatu mbele ya Sailors.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako