• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Solskjaer ahakikishiwa kibarua chake

  (GMT+08:00) 2019-12-11 18:32:41

  Wamiliki wa timu ya Manchester United, familia ya Glazer, imemuhakikishia kocha wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer kibarua chake kuwa sehemu salama baada ya ushindi wa wiki iliyopita dhidi ya timu kubwa nchini England. Kocha huyo alipewa michezo miwili kuweza kuokoa kibarua chake wiki iliyopita, mchezo dhidi ya Tottenham inayofundishwa na kocha wa zamani wa United, Jose Mourinho pamoja na mchezo mwingine dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City ikiwa chini ya kocha Pep Guardiola. Mchezo wa kwanza ulipigwa kwenye uwanja wa Old Ttafford dhidi ya Tottenham na Manchester United ikafanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1, huku mchezo uliofuata dhidi ya Manchester City kwenye Uwanja wa Etihad na Manchester United ikashinda mabao 2-1.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako