• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Pellegrini: Mimi ni kocha sahihi West Ham

    (GMT+08:00) 2019-12-11 18:32:57
    Mbali na timu ya West Ham kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Arsenal, juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini, amedai bado yeye ni mtu sahihi wa kuisimamia timu hiyo. West Ham walikubali kichapo hicho kwenye uwanja wa nyumbani mabao yakifungwa na Gabriel Martinelli, Nicolas Pepe na Pierre Aubameyang, jambo ambalo limemfanya kocha huyo kuendelea kuwa katika wakati mgumu wa kulinda kibarua chake. Lakini kocha huyo anaamini mbali na kuchezea kichapo bado ana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko ya matokeo hayo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako