Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema, Marekani haina mamlaka ya kuzungumzia hali ya haki za binadamu nchini China.
Bibi Hua amesema hayo alipoulizwa kuhusu kauli ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ya kuilaumu China kuwakandamiza watu wenye dini na wa makabila madogo, na kunyima uhuru wa wananchi.
Amesema Marekani yenyewe inakabiliwa na changamoto kubwa ya haki za binadamu haswa ubaguzi wa rangi, na mara kwa mara inaingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kufanya vita katika nchi kadhaa ikiwemo Iraq, Syria, na Afghanistan, na kuua watu wengi wasio na hatia, hivyo haina haki ya kulalani hali ya haki za binadamu ya nchi nyingine.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |