• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KASHFA: Malinzi na Mwesigwa wahukumiwa miaka miwili jela au faini sh. 500,000

  (GMT+08:00) 2019-12-12 10:03:32

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha miaka miwili gerezani au faini ya Sh. 500,000 aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kwa mashitaka ya kughushi nyaraka za muhtasari wa kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo. Aidha, aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amekutwa na mashitaka mawili; kughushi nyaraka za kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo na kutengeneza nyaraka za uongo, hivyo kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya Sh. 1,000,000. Wote wawili wamekubali kulipa faini, lakini ofisi zilikuwa zimekwishafungwa hivyo wamerudishwa rumande na zoezi hilo litafanyika leo ndipo wataachiwa huru.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako