• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Gennaro Gattuso achukua mikoba ya Carlo Ancelotti klabu ya Napoli

  (GMT+08:00) 2019-12-12 10:03:58

  Gennaro Gattuso jana alichukua mikoba ya Carlo Ancelotti na kuwa kocha mpya wa Napoli baada ya Ancelotti kufukuzwa kazi licha kuiongoza klabu kuingia kwenye 16 bora ya Champions League. Gattuso, aliyeondoka AC Milan mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu Champions League, atawafunda Napoli waliopo nafasi ya saba kwenye Serie A. Akieleza mikakati yake kwenye klabu yake mpya, Gattuso, aliyeshinda kombe la dunia mwaka 2006 akiwa kama mchezaji wa timu ya taifa ya Italia, amesema lengo ni kurejesha pointi na kurejea kwenye nafasi nzuri ya Champions League, na kuahidi kujituma Zaidi ili kurejesha pointi hizo na kuiweka klabu katika nafasi nzuri. Kocha huyo mpya mwenye miaka 41 anachukua nafasi ya Ancelotti, aliyemfunza Gattuso na kushinda mataji mawili ya Champions Leagues na moja la Serie A kwa Zaidi ya miaka minane akiwa na Milan ambao ni mabingwa mara 7 wa Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako