• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MASUMBWI: Bondia Dillian Whyte arejeshwa tena rasmi katika WCB mashataka yake yafutwa

  (GMT+08:00) 2019-12-12 10:04:51

  Bondia wa uzito wa juu wa Uingereza Dillian Whyte amerejeshwa tena rasmi katika ngumi za uzito wa juu duniani za Deontay Wilder's World Boxing Council. Hatua hiyo imekuja baada ya Whyte, mwenye miaka 31, kufutiwa mashtaka ya kutumia dawa za kusisimua misuli. Mwezi Juni, alitoa sampuli ambayo ina alama ya dawa zilizopigwa marufuku ya steroid. Lakini Mamlaka Inayopambana na dawa kusisimua misuli ya Uingereza imemfutia mashtaka kwa vile kiwango kilikuwa kidogo sana. Sasa Whyte anaweza kupambana na mshindi wa Wilder Tyson Fury. POambano linapangwa kufanyika February 2020 nchini Marekani, huku WBC ikisema Whyte atapambana kuwania taji la dunia kwa mara ya kwanza mwezi Februari 2021.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako