• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Feri tatu zapigwa marufuku kuhudumu Likoni

    (GMT+08:00) 2019-12-12 18:37:06

    Bunge la Kenya limepitisha pendekezo la kutaka feri tatu zipigwe marufuku kuhudumu nchini Kenya hali ambayo huenda ikasababisha tatizo kubwa la uchukuzi katika kivuko cha feri cha Likoni mjini Mombasa.

    Ripoti ya kamati ya kuhusu Uwekezaji wa Umma iliyochunguza usalama wa wasafiri wanaotumia kivuko hicho, ilisema feri hizo ambazo zimehudumu kwa zaidi ya miaka 20 si salama kwa wasafiri.

    Kufuatia hatua ya wabunge kukubali utekelezaji wa yaliyomo kwenye ripoti hiyo, Mamlaka ya Usafari wa Majini (KMA) sasa inatarajiwa kufutilia mbali leseni za feri zote ambazo hazijatimiza viwango vinavyohitajika vya usalama.

    Ripoti ya kamati hiyo ilipata kuwa feri tatu zimehudumu kwa miaka 30 kinyume cha sera za Shirika la Huduma za Feri, ambazo zinasema kwamba chombo hicho cha usafiri kinafaa kubadilishwa baada ya miaka 20.

    Hivi sasa kuna feri sita pekee ambazo zinahudumu katika kivuko cha likoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako