• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege ya Tanzania yaachiliwa nchini Canada

    (GMT+08:00) 2019-12-12 18:37:26

    Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imekamatwa nchini Canada imeachiliwa na wananchi wajiandae kuipokea katika Uwanja wa Ndege jijini Mwanza.

    Akizungumza mjini Mwanza, Rais Magufuli amesema wananchi wa Tanzania watatangaziwa tarehe rasmi ya kuwasili kwa ndege hiyo. Novemba 23, 2019, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi alitangaza kukamatwa kwa ndege hiyo kufuatia kesi iliyowasilishwa mahakamani na mfanya biashara mmoja nchini Afrika kusini anayefahamika kama Hermanus Steyn akidai fidia ya dola 33 milioni. Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019.

    Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako