• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa kahawa walalamikia bei ndogo ya bidhaa hiyo

    (GMT+08:00) 2019-12-12 18:38:27

    Wadau wa kahawa nchini, wasema bei ndogo ya zao hilo katika soko la dunia hasa ile inayostawishwa Tanzania ni moja ya mambo yanayokwamisha jitihada za serikali kufufua kasi ya uzalishaji wake.

    Mabadiliko ya tabia nchi nayo yanatajwa kuwa moja ya matatizo ambayo yanaikabili sekta hiyo kwa sasa.

    Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wadau wa Kahawa Tanzania, Noel Yatera, amesema zinahitajika jitihada za makusudi kuhakikisha wakulima wanapata masoko ya uhakika na bei nzuri ya kahawa licha ya kuwapo kwa matatizo hayo.

    Alisema kwa miaka mitatu sasa, bei ya kahawa nje ya nchi imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.

    Ameongeza kuwa hali hiyo ndiyo inayochangia kupungua kipato cha wakulima na kufanya wengi kukimbia kilimo hicho, huku uzalishaji ukiendelea kuwa wastani wa tani 50 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako