• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa China nchini Kenya watoa zawadi za mwaka mpya kwa watoto wa shule ya mtaa wa Mathare

    (GMT+08:00) 2019-12-12 18:51:49

    Ubalozi wa China nchini Kenya umetoa zawadi za mwaka mpya kwa watoto wa shule ya Mcedo-Beijing iliyoko kwenye mtaa wa Mathare. Zawadi hizo ikiwa ni pamoja na chakula na vifaa vya michezo zimewafurahisha sana watoto hao.

    Mathare ni mtaa wa pili wa makazi duni kwa ukubwa nchini Kenya. Shule ya Mcedo-Beijing ya mtaa huo ilijengwa mwaka 2007 kwa kufadhiliwa na ubalozi wa China. Hivi sasa shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 500, na Selvin Kasowa ni mmoja wao, anasema,

    "Nilizaliwa na kukua hapa Mathare, na ndugu zangu wawili wanasoma katika shule hiyo. Tunahitaji kufanya juhudi kwa ajili ya maisha, na kwa ajili ya malengo yetu."

    Ndoto ya Kasowa ni kuwa mchezaji wa soka. Sasa yeye ni mwanachama wa Klabu ya soka ya shule ya Mcedo-Beijing. Mara hii ubalozi wa China ulichangia shule hiyo vifaa vya soka venye thamani ya dola karibu elfu 3 za kimarekani. Hali hii inamfurahisha sana kwani atakuwa na viatu na nguo mpya za kuchezea soka. Anasema,

    "Soka inanisaidia kusahau changamoto za kimaisha. Hivyo tunataka kushukuru makocha wetu kwa kutuunga mkono kucheza soka. Leo mmetuletea vifaa vya soka, pia tunawashukuru sana."

    Kutokana na msaada wa China, klabu ya soka ya Kasowa ilipewa jina la "Washambulizi wa Beijing". Klabu hiyo ilifanikiwa kuingia michezo ya kitaifa ya soka. Mkuu wa shule ya Mcedo-Beijing Benedict Kiage amesema, soka inamaanisha ndoto na mabadiliko kwa wasichana wa mtaa wa Mathare. Anasema,

    "Tuna timu ya soka ya wanawake, ambao wanafundisha wasichana namna ya kucheza soka. Kucheza soka kunaweza kuwasaidia kujiunga na shule. Hivyo tunawashukuru ninyi kutusaidia mipira na vifaa vingine ya soka."

    Bw. Kiage alikulia kwenye mtaa wa Mathare, na baada ya kuhitimu masomo yake alirudi huko kuwa mwalimu, kwani anaona, elimu inaweza kubadilisha mustakabali wa watu, haswa watoto maskini. Amesema watoto wa shule yake wanapenda kujua dunia ya nje,

    "Nataka kusema watoto wa mtaa wa makazi duni wanapenda kusherehekea sikukuu pamoja na watu kutoka nje. Hivyo wanafurahia sana watu wa ubalozi wa China kuja hapa wakiwa na zawadi."

    Konsela wa uchumi na biashara wa ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce amesema, licha ya vifaa ya michezo, pia wamefadhili watoto wa shule hiyo chakula cha asubuhi na mchana kwa mwaka mmoja. Aidha ameeleza matumaini yake kwamba makampuni ya China nchini Kenya yatatekeleza vizuri majukumu ya kijamii. Anasema,

    "Naamini chakula cha bure kitakidhi mahitaji ya ukuaji wa mwili wa watoto hao. Msaada huo umetolewa na Shirikisho la Makampuni ya China nchini Kenya, pamoja na Kampuni ya Startimes na Kampuni ya Mawasiliano ya Habari ya China. Baadaye tutaendelea kuhamasisha makampuni ya China nchini Kenya kuzingatia majukumu ya kijamii, haswa maisha ya watoto kwenye mitaa ya makazi duni."

    Kasowa amesema, ingawa shule yake inaitwa Shule ya Mcedo-Beijing, lakini hajapata nafasi ya kwenda China, na anatumai kutembelea Beijing siku moja. anasema,

    "Natumai nitaweza kwenda Beijing, hivyo nitakuwa na marafiki wengi zaidi wa China. Wao ni wazuri sana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako