• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kongamano la Haki za Binadamu la Kusini-Kusini lasisitiza kushikilia anuwai ya ustaarabu wa binadamu

  (GMT+08:00) 2019-12-12 19:01:31

  Kongamano la mwaka 2019 wa la Haki za Binadamu la Kusini-Kusini umemalizika jana hapa Beijing.

  Naibu mkuu wa taasisi ya haki za binadamu ya China Bw. Li Junru amesema, nchi zinazoendelea zinakabiliwa na matatizo mawili katika maendeleo ya haki za binadamu, idadi kubwa ya watu na hali duni ya maendeleo ya uchumi. Amesema mwaka ujao, China inadhamiria kukamilisha lengo la kuondoa umaskini, na hayo ni mafanikio ya kihistoria ya maendeleo ya haki za binadamu ya China.

  Mtendaji wa chama tawala cha Kenya anayeshughulikia mambo ya siasa Bw. Kadara Harth Swaleh amesema, nchi mbalimbali zinapaswa kuzingatia hali halisi na asili ya utamaduni wakati wa kuendeleza kazi ya haki za binadamu.

  Naye Mjumbe maalumu wa wizara ya mambo ya nje ya China anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu Bw. Liu Hua amesema, kila mtu ana hamu ya kufurahia haki za binadamu, lakini siyo jambo la kipekee la nchi chache. Nchi zinazoendelea siku zote ni nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya haki za binadamu duniani.

  Mwenyekiti wa kamati ya haki za binadamu ya Niger ambaye pia ni rais wa zamani wa Niger Bw. Halid Ikhiri amesema, ugaidi ni adui wa jamii, na kuongeza kuwa Niger inasumbuliwa sana na ugaidi, ambao unazuia maendeleo ya nchi nyingi zilizoko nyuma kimaendeleo. Kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi katika mkoa wa Xinjian nchini China, Bw. Ikhiri amesema mkoa wa Xinjiang ni kituo muhimu cha kupambana na ugaidi kwa China, na kazi ya kupambana na ugaidi katika mkoa huo ni muhimu sana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako