• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kocha Mourinho amshirikisha Victor Wanyama katika mechi dhidi ya Bayern Munich

  (GMT+08:00) 2019-12-12 19:26:02

  Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars anayechezea klabu ya Tottenham Hotspurs Victor Wanyama anatazamiwa kushiriki katika mechi ya klabu kwa mara ya kwanza dhidi ya Bayern Munich. Wanyama alikuwa miongoni mwa kikosi kilichokwenda Ujerumani jana kwa mechi kubwa ya Kundi B. Tangu kuteuliwa kwake mwezi Novemba, Mourinho amefufua makali ya Spurs huku akishinda mechi nne kati ya tano. Hata hivyo, uongozi wake umeleta afueni kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Wanyama, ambaye alikuwa anaonekana amepoteza nafasi yake kwa Harry Winks na Moussa Sissoko. Katika mechi hiyo, Bayern Munich waliibuka kidedea kwa kuichapa Spurs mabao 3 – 1.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako