• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Lampard anogesha vita ya kumnasa Sancho

  (GMT+08:00) 2019-12-12 19:26:22

  Frank Lampard amesisitiza kuwa Chelsea itafanya kila inaloweza kumnasa Jadon Sancho kwenye dirisha la usajili litakalofunguliwa Januari klwa ada inayodaiwa kuwa ni pound milioni 100. Sancho mwenye umri wa miaka 19 anayechezea klabu ya Borussia Dortmund, aliendelea kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Slavia Prague iliyochezwa jumanne usiku, na mpaka sasa amefunga mabao matano na kusaidia mara nne katika mechi sita za mwisho. Chelsea inayomwinda kinda huyo, haijapata mtu wa kuziba pengo la Eden Hazard tangu alipoondoka kwenye dirisha lililopita, kitu kinachomfanya kocha Lampard kuamini Sancho anaweza kumaliza tatizo hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako