• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mason Greenwood aisaidia Manchester United kuichakaza AZ Alkmaar 4-0 Europa League

  (GMT+08:00) 2019-12-13 08:57:02

  Mason Greenwood ameifungia Manchester United mabao mawili huku timu yake ikipata mbao 4 ndani ya dakika 11 na kuichakaza vibaya AZ Alkmaar ambayo haikuondoka hata na goli la kufutia machozi. Ushindi huo umeipaisha juu Manchester United na kuingia hatua ya mtoano ya 32 bora ya UEFA Europa League. Baada ya kipindi cha kwanza kilichodorora, michuano ilipata uhai katika dakika ya 53 baada ya Ashley Young kuitumia vizuri krosi ya Juan Mata na kupachika goli lake la kwanza tangu Februari. Hata hivyo Greenwood ametawala vichwa vya habari baada ya kufunga mabao mawili dakika ya 58 na 64. Hii ni mara ya kwanza kwa kinda huyo mwenye miaka 18 kufunga mabao mawili katika kikosi cha kwanza na kufanya kuwa na jumla ya mabao 6 katika msimu. Greenwood sasa ndio mfunga magoli anayeongoza wa United katika michuano ya Ulaya msimu huu huku Marcus Rashford akiwa na magoli mengi zaidi katika michuano yote. Mabao mengine ya Man United yamefungwa na Ashley Young dakika ya 53 na Juan Mata dakika ya 62 kwa penalty.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako