• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ferrari yakiri kufanya mazungumzo na Lewis Hamilton kuhusu kujiunga nao siku za mbele

  (GMT+08:00) 2019-12-13 08:57:21

  Ferrari wamekiri kwamba walifanya mazungumzo na bingwa wa dunia Lewis Hamilton kuhusu kujiunga nao siku za mbele. Afisa mtendaji mkuu wa Ferrari Louis Carey Camilleri amesema Hamilton alifanya mazungumzo na mwenyekiti John Elkann. Camilleri amesema Ferrari imevutiwa Zaidi na Lewis na madereva wengine pia wanataka kujiunga nao. Hata hivyo amesema mazungumzo bado ni machanga na ikifikia muda wataangalia nani anayefaa zaidi. Hamilton, ambaye mwezi ujao anatimiza miaka 35 na ambaye anatarajiwa kuanza kampeni zake za kulisaka taji la saba duniani mwaka 2020, anamaliza mkataba wake na Mercedes msimu ujao. Kwa sasa Hamilton hajakubali wala kukataa kuhusiana na ripoti za Italia kwamba alifanya mazungumzo mara mbili mwaka huu na Elkann.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako