• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kocha mpya Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck aahidi makubwa kwa Simba SC

  (GMT+08:00) 2019-12-13 08:57:37

  Kocha mpya wa Simba SC, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck ameahidi kuipa klabu hiyo mafanikio makubwa kisoka kwa kushinda nyumbani na kufanya vyema kwenye michuano ya Afrika. Vandenbroeck amesema amevutiwa na Simba SC kutokana na kuwa na mashabiki wengi. Amesema ni jambo la kufurahisha kuona mashabiki 60,000 wakishangilia inatoa hisia za kipekee. Amefafanua kuwa lengo la kwanza ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu, na pia kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya CAF. Vanderbroeck, mwenye umri wa miaka 40 amejiunga na Simba SC baada ya kuachana na timu ya taifa ya Zambia na atakuwa anasaidiwa na kiungo na Nahodha wa zamani wa klabu hyo Suleiman Matola.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako