• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mbio za Marathon katika Olimpiki ya walemavu zitasalia Tokyo

  (GMT+08:00) 2019-12-13 08:58:14

  Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu IPC imesema mbio za Marathon katika Olimpiki ya walemavu ya Tokyo mwakani hazitahamishiwa mji mwingine. Olimpiki ya walemavu itafanyika kuanzia Agosti 25 hadi Septemba 6. Rais wa IPC Andrew Parsons amesema wanariadha wengi walemavu wanataka michuano yao ibakie Tokyo. Mbio tano za marathon zitafanyika kwenye michuano ya walemavu ya Tokyo 2020. Bw. Parsons amesema kulingana na data za hali ya hewa zilizoangaliwa na kamati ya matibabu ya IPC, zinaonesha kuwa ingawa kipindi cha michuano ya mwaka huu kilikuwa na joto kidogo kuliko mwaka 2018, lakini joto katika kipindi ambacho michezo ya Olimpiki itafanyika litakuwa salama kwa wachezaji kwenye mashindano. Ikumbukwe kuwa mbio za Marathon na kutembea kwa kasi kwenye olimpiki ambazo zitaanza Julai 24 hadi Agosti 9 zimehamishiwa Sapporo kwasababu ya hofu ya joto kali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako