• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kenya yapigwa mkwara mapema

  (GMT+08:00) 2019-12-13 18:45:28

  Wenyeji Uganda imekuwa timu ya kwanza ya Kundi A kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Challenji 2019, kama ilivyokuwa kwa Kenya waliopenya mapema kutoka kundi B, huku wakitamba kuwa wako tayari kukutana na wenyeji hao katika hatua yoyote. Upo uwezekano wa Kenya na Uganda kukutana katika hatua ya nusu fainali ikiwa Kenya itapoteza mchezo wa mwisho kesho dhidi ya Zanzibar na Tanzania Bara ikaibuka na ushindi wa idadi nzuri ya magoli dhidi ya Sudan. Kocha wa Uganda Jonathan McKindtry amesema haogopi kasi ya Kenya katika kundi B na hana wasiwasi wa kukutana nao katika hatua zinazofuata.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako