• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Mwakinyo apanda viwango vya dunia

  (GMT+08:00) 2019-12-13 18:46:00

  Siku chache baada ya kumchapa Arnel Tinampay wa Philippines kwa pointi, bondia Hassan Mwakinyo wa Tanzania amepanda kwa nafasi mbili kwenye viwango vya ngumi vya dunia katika uzani wa Super Welter. Katika viwango hivyo vinavyotolewa na mtandao wa ngumi wa dunia, Mwakinyo amepanda hadi nafasi ya 17 kutoka nafasi ya 19 aliyokuwa awali. Mtanzania huyo mwenye nyota nne kati ya tano ambazo ni za kiwango cha juu na cha mwisho katika ngumi za kulipwa, licha ya kupanda hadi nafasi ya 17, ameendelea kuwa namba moja Afrika kwenye uzani huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako