• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Amri Saidi kuanza na Yanga Mbeya City

  (GMT+08:00) 2019-12-13 18:46:45

  Licha ya awali kuelezwa yuko mbioni kuingia mkataba na Ndanda FC, aliyekuwa kocha wa Biashara United, Amri Saidi, amesaini mkataba wa miezi sita wa kuinoa Mbeya City ya jijini Mbeya. Kutokana na mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu yaliyotolewa na Bodi ya Ligi, Said ataanza kuiongoza timu hiyo kwa kuialika Yanga kwenye Uwanja wa Sokoine Desemba 24 mwaka huu. Kocha huyo amesema anatarajia kuanza alipoishia aliyekuwa kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi aliyejiuzulu hivi karibuni, na kwamba mkakati wake ni kukiboresha kikosi hicho kuelekea dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kugunguliwa jumatatu ijayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako