• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ofisa mwandamizi wa CPC asisitiza maendeleo ya amani ya China kwenye siku ya kukumbusha mauaji ya Nanjing

  (GMT+08:00) 2019-12-13 18:57:14

  Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Huang Kunming amesema, China inapenda kudumisha njia ya amani ya maendeleo.

  Bw. Huang alisema hayo alipohutubia kwenye hafla ya kukumbusha mauaji ya Nanjing, mkoa wa Jiangsu, ambapo watu laki 3 waliuawa na wavamizi wa Japan katika vita kuu ya pili duniani. Bw. Huang amesema, watu wa China wamedhamiria kutunza historia hiyo, kutosahau mambo yaliyopita, kuthamini amani, na kuendelea kujenga siku nzuri za usoni. Amesema, wahanga na watu waliojitoa muhanga wataridhishwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana na watu wa China ya kujiendeleza na ustawi chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China katika miongo iliyopita, tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949. Pia amesema, hakuna nguvu yoyote inayoweza kuwazuia watu na taifa la China kuendelea kupiga hatua.

  Habari zinasema, vijana 82 wamesoma azimio la amani kwenye Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na watu elfu 8 kutoka sekta mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako