• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marufuku kuagiza magunia ya Korosho kutoka nje 2020

    (GMT+08:00) 2019-12-13 19:01:18

    Serikali ya Tanzania imesema kuanzia mwaka 2020 haitaruhusiwa magunia ya korosho kutoka nje kuingia nchini humo. Naibu Waziri wa Kilimo nchini humo Bw Hussein Bashe amesema badala yake bidhaa hiyo itatengenezwa na viwanda vya ndani.

    Amesema hayo kwenye mkutano na wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora akihamasisha zao la korosho wilayani humo.

    Amesema kutokana na viwanda vya ndani kuwa na uwezo wa kutengeneza magunia yanayoweza kutosheleza mahitaji hakutakuwa na haja ya kuagiza kutoka nje.

    Mwaka huu pekee Tanzania imeagiza magunia kwa ajili ya korosho yenye thamani ya Sh16 bilioni. Amesema kuwa kuingiza magunia kutoka nje ya nchi ni gharama ikilinganishwa na yanayotengenezwa nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako