• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usafirishaji wa mafuta wakatizwa kwa siku 10 Kenya

    (GMT+08:00) 2019-12-13 19:01:33

    Usafirishaji wa mafuta ghafi katika eneo la Turkana nchini Kenya umekatizwa kufuatia kuharibika kwa barabara katika eneo hilo. Hata hivyo kampuni ya Tullow ambayo inasafirisha mafuta hayo kwa kutumia malori haijasema ni kwa kiwango gani mkatizo huo utakavyoathiri shughuli hiyo ya usafirishaji lakini maofisa ndani ya kampuni hiyo wanasema shughuli za usafiri zimekatizwa kwa takriban siku 10 hivi.Wizara ya madini na mafuta ya Kenya imesema mipango iko njiani ya kuongeza mara mbili usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Turkana katika robo ya kwanza kuanzia mwaka ujao.Kenya ilikuwa imepanga kusafirisha mapipa laki tano ya mafuta ghafi ifikapo machi mwaka ujao ikiwa ni mara mbili ya mapipa yaliyosafirishwa katika mwezi wa Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako