• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri ahimiza nishati gesi asilia

  (GMT+08:00) 2019-12-13 19:02:10

  Serikali ya Tanzania imewataka wawekezaji, wafanyabiashara na wananchi wote kuanza kutumia nishati ya gesi inayopatikana nchini humo ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira.

  Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makumu wa Rais nchini humo Bw Musa Sima amesema wakati umefika kwa viwanda kujikita katika matumizi ya nishati ya gesi.

  Amesema hatua hiyo pia itasaidia kupunguza ongezeko la hewa ukaa na pia kulinda mazingira na kuongeza kuwa ni jukumu la wawekezaji na wafanyabiashara kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ili kujenga miundombinu ya kufikisha gesi hiyo katika maeneo husika ili ianze kutumia.

  Amesisitiza kuwa maendeleo ya ukuaji wa uchumi na viwanda yatakuwa na maana kubwa kama kutakuwa na uzingatiaji wa kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na matumizi ya nishati ya gesi ambayo ni rafiki kwa mazingira.

  Alisema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na utoaji wa vibali vinavyohusiana na uwekezaji kwa wakati ili kutokwamisha azma ya serikali ya kujenga uchumi wa kazi na viwanda ifikapo 2025.

  Pia amewataka wawekezaji wa viwanda kuwa na vitalu vya miti katika maeneo yao kama sehemu ya kuendelea kutunza mazingira na utekelezaji wa kanuni na Sheria ya Baraza laTaifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) la kuwataka wenye viwanda kuwa na vitalu vya kuotesha miti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako