• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yakana kuona nia nzuri ya Marekani kutokana na vitendo vyake

  (GMT+08:00) 2019-12-13 19:47:54

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema China haijaona nia nzuri ya Marekani kutokana na vitendo na kauli zake mbaya.

  Bibi Hua amesema hayo baada ya msaidizi waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia mambo ya Asia na Pasifiki David Stilwell kusema hivi karibuni kuwa, Marekani inasikitishwa na jinsi China inavyojibu vibaya msaada mkubwa uliotolewa na Marekani kwa nchi hiyo katika miongo kadhaa iliyopita.

  Hua amesema kauli hiyo haiendani na hali halisi na inajaribu kuhalalisha sera mbaya inayotekelezwa sasa na Marekani kwa China. Amesema China haijatendewa vyema na Marekani baada ya nchi hiyo kutoa masharti na changamoto kwa China bila ya sababu katika maeneo kadhaa ikiwemo uchumi na biashara, teknolojia na mawasiliano ya watu, kuchafua jina la China katika masuala ya Hong Kong, Taiwan, Xinjiang, na maeneo mengine yanayohusu maslahi makuu ya China ukiwemo ukamilifu wa ardhi na heshima ya taifa. Mbali na hayo, Marekani pia inatumia majukwaa mbalimbali ya kimataifa kukosoa mfumo wa kijamii na njia ya kujiendeleza ya China na ushirikiano kati ya China na nchi nyingine.

  Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi leo hapa Beijing amesema, China inaitaka Marekani ijenge mtazamo sahihi kuhusu China na dunia, pia kushirikiana na China katika kutimiza malengo ya kutopambana, kuheshimiana na kushirikiana. Pia kutafuta njia ya kuishi kwa amani na ushirikiano wa kusaidiana kati ya nchi hizo mbili ambazo zina mifumo tofauti ya kijamii, njia tofauti za kujiendeleza na historia na ustaarabu tofauti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako