• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuimarisha hatua za kulinda maslahi ya wawekezaji wa nje

  (GMT+08:00) 2019-12-13 20:50:25

  China itaimarisha hatua za kuvutia na kulinda uwekezaji wa nje mwakani.

  Hayo yamesemwa kwenye muswada wa taratibu za utekelezaji wa sheria ya uwekezaji wa nje ya China uliopitishwa leo kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri ulioendeshwa na waziri mkuu Bw. Li Keqiang. Muswada huo utaanza kutekelezwa Januari Mosi, mwakani.

  Taratibu hizo ni pamoja na kutendea kwa usawa kampuni za ndani na za nje, kupiga marafuku hatua za kulazimisha wawekezaji na kampuni za nje kukabidhi teknolojia, kutotumia masharti yenye upendeleo katika kushughulikia maombi ya wawekezaji wa nje ya kuingia kwenye sekta fulani, na pia kuweka wazi adhabu za kisheria zitakazotolewa kwa vitendo vinavyokiuka taratibu hizo.

  Mkutano huo umesema, China inatekeleza vizuri sheria ya uwekezaji wa nje na taratibu hizo na kuanda mazingira ya soko yasiyo na upendeleo, yenye haki na ushindani kwa kampuni za ndani ya nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako