• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia itatoa uungaji mkono mkubwa kwa uwekezaji kutoka China

  (GMT+08:00) 2019-12-14 17:10:35

  Rais Salhe Work Zewde amesema Ethiopia itatoa uungaji mkono mkubwa kwa uwekezaji wa China nchini Ethiopia.

  Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Ethiopia inasema, Rais Zewde amepongeza uwekezaji mkubwa wa China uliopo nchini mwake, na kusema Ethiopia itaendelea kuvutia zaidi uwekezaji kutoka China. Taarifa hiyo imetolewa baada ya ziara ya ujumbe wa wafanyabiashara wa China kwenye jumba la taifa mjini Addis Ababa.

  Mkuu wa idara ya mawasiliano na umma wa Tume ya Uwekezaji ya Ethiopia (EIC) Bw Mekonen Hailu, amesema Ethiopia imevutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka China wenye thamani ya dola milioni 700 katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, na kuwa nchi iliyovutia zaidi uwekezaji kutoka China.

  Makampuni ya China yanawekeza zaidi kwenye sekta ya viwanda, ikifuatiwa na sekta za huduma na kilimo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako