• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yawa mwenyeji wa baraza la ushirikiano wa nishati kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-12-14 17:11:06

    Kenya imekuwa mwenyeji wa baraza la nishati kati ya China na Afrika kujadili ushirikiano kwenye sekta ya nishati kati ya pande hizo mbili chini ya utaratibu wa "ukanda mmoja, njia moja".

    Baraza hilo ambalo ni la kwanza la aina yake liliandaliwa jana na jumuiya ya washauri bingwa ya Sera za Afrika, kwa ushirikiano na shirika kubwa la mafuta la China CNPC. Wahudhuriaji ni pamoja na wanadiplomasia wa China na Afrika, watunga sera, wakuu wa viwanda na wasomi, wakijadili fursa kwenye soko la nishati barani Afrika, zinazoweza kuhimiza ongezeko la uchumi wa Afrika.

    Balozi wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng amesema China iko tayari kushiriki kwenye maendeleo ya sekta ya nishati barani Afrika kwa mujibu wa pendekezo la "ukanda mmoja, njia moja", na kusema ushirikiano kwenye sekta hiyo kati ya China na Afrika kimsingi ni wa kunufaishana. Amesema kwa sasa makampuni ya China yanashiriki zaidi kwenye maeneo ya nishati ya upepo na jua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako