• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makubaliano ya awali ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani yasaidia uchumi wa dunia

  (GMT+08:00) 2019-12-14 17:34:25

  Kutokana na juhudi za pamoja za ujumbe wa uchumi wa China na Marekani, na kwa msingi wa usawa na kuheshimiana, China na Marekani zimeafikiana kuhusu makubaliano ya awali ya kiuchumi na kibiashara. Hayo ni matunda yaliyopatikana baada ya mazungumzo yaliyoendelea kwa miezi 22.

  Marekani itatimiza ahadi yake hatua kwa hatua kuondoa ushuru wa forodha ilioongeza dhidi ya bidhaa za China. Kuhusu hilo naibu waziri wa fedha wa China Bw. Liao Min alisema,

  "kuondoa ushuru wa forodha ni jambo linalofuatiliwa na China katika mazungumzo ya biashara. Marekani imeahidi kuondoa baadhi ya ushuru wa forodha unaopangwa kuongezwa na ulioongezwa, na kuongeza nguvu katika kusamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa za China. Vilevile, China pia inafikiri kutotekeleza hatua zilizopangwa kutekelezwa kuanzia tarehe 15 Desemba za kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za Marekani."

  Kwa upande wa chakula na kilimo, naibu waziri wa kilimo wa China Bw. Han Jun alisema, China itaongeza kuingiza bidhaa za kilimo kutoka Marekani kwa kiasi kikubwa.

  "makubaliano hayo yakitekelezwa, China itaongeza kwa kiasi kikubwa manunuzi ya mazao ya kilimo kutoka Marekani, ambayo yatasaidia kupunguza ukosefu wa mazao ya kilimo nchini China. Kwa mfano, China inaingiza maharage karibu tani milioni 90 kila mwaka, na hivi karibuni China imetangaza kuondoa vikwazo vya kununua nyama ya nguruwe na ya ndege kutoka Marekani. Pia China itanunua ngano, mahindi na mchele kutoka Marekani, ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani. "

  Habari zinasema katika kipindi kijacho China na Marekani zitakamilisha uthibitishaji wa kisheria wa makubaliano hayo, kuyatafsiri na mchakato mwingine haraka iwezekanavyo, na kushauriana mpango wa kusaini rasmi makubaliano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako