• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa kilimo wa Marekani wakaribisha China na Marekani kufikia makubaliano ya awali ya kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-12-14 17:43:26

    Mashirika ya kilimo ya Marekani na wakulima wamekaribisha China na Marekani kuafikiana kuhusu nakala ya makubaliano ya awali ya kiuchumi na kibiashara, wakitumai kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa haraka iwezekanavyo, na uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili utarudi kwenye njia sahihi.

    Mwenyekiti wa shirika la maharage la Iowa, jimbo maarufu kwa kilimo, Bw. Tim Badal amlisema,

    "nimefurahi kusikia China na Marekani zimefikia makubaliano. Katika miaka ya hivi karibuni tumepoteza fedha za kulima maharage, tunatumai kuanzia sasa tunaweza kupata uwiano katika mapato na matumizi na kuanza kupata faida. Tunatumai makubaliano hayo yatatekelezwa haraka iwezekanavyo, na biashara ya mazao ya kilimo ifanywe katika hali ya kawaida kati ya nchi hizo mbili."

    Naibu mwenyekiti mtendaji wa shirika la wakulima wa nafaka la jimbo la Montana Bibi Laura Lashkar alisema,

    "tumefurahia sana habari hii, inatutia moyo kweli. Tunataka makubaliano hayo yatatekelezwa haraka. Katika muda zaidi ya mwaka mmoja uliopita China na Marekani zimepata changamoto nyingi kuhusu suala la uchumi na biashara. Tunatumai changamoto hizo zitatatuliwa haraka."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako