• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zafikia makubaliano ya awali ya kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-12-14 18:07:12

    China na Marekani zimekubaliana kuhusu nakala awali ya makubaliano ya kiuchumi na kibiashara. Taarifa iliyotolewa hivi punde na China inasema, makubaliano hayo yamefikishwa kwa msingi kanuni za kuwa usawa na kuheshimiana. Imefahamika kuwa makubaliano hayo yana sehemu tisa zikiwemo utangulizi, hakimiliki ya kiujuzi, chakula na mazao ya kilimo, huduma za fedha, kiwango cha ubadilishaji wa fedha na uwazi wake, upanuazi wa biashara, tathmini na utatuzi wa mikwaruzano, na vipengele vya mwisho. Vile vile nchi hizo mbili zimekubaliana kuwa, Marekani itatekeleza ahadi ya kuondoa hatua kwa hatua ushuru wa forodha ilioongeza dhidi ya bidhaa zilizotengenezwa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako