• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuahirisha hatua za kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani

    (GMT+08:00) 2019-12-15 15:54:03
    Ili kutekeleza matokeo ya hivi karibuni ya mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani, kwa mujibu wa sheria ya forodha ya China, sheria ya biashara ya nje ya China, kanuni ya ushuru wa biashara ya kununua na kuuza bidhaa ya China na sheria nyingine pamoja na kanuni ya kimsingi ya sheria ya kimataifa, kamati ya ushuru ya baraza la serikali la China imeamua kuwa, kuanzia saa 6 na dakika 1 mchana wa tarehe 15 Disemba, China itasitisha kuongeza ushuru wa asilimia 10 na asilimia 5 kwa baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na Marekani, na kusimamisha kuongeza ushuru kwa magari na vipuri vya magari kutoka Marekani.

    Licha ya hatua hizo, hatua nyingine za kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani zitaendelea, kazi ya kuondoa ushuru kwa bidhaa za Marekani itaendelea.

    China inatumai juu ya msingi wa usawa na kuheshimiana China na Marekani zitashirikiana kutatua masuala yanayofuatiliwa na pande zote mbili, ili kuhimiza maendeleo ya utulivu ya uhusiano wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako