• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TUZO: Eliud Kipchoge awa mfalme wa taji la BBC la mwanaspoti bora wa mwaka

  (GMT+08:00) 2019-12-16 08:48:33

  Mfalme wa mbio za Marathon Eliud Kipchoge amewabwaga wanaspoti mahiri duniani kunyakua taji maridadi la BBC la kuwa Mwanaspoti Bora wa mwaka Duniani. Kipchoge amekuwa na wakati mzuri mwaka 2019, hususan alipoandika historia yake katika kivumbi cha INEOS 1:59 aliposhuhudiwa kuwa mtu wa kwanza kumaliza mbio za marathon chini ya saa mbili mwezi Oktoba. Kufaulu kwake kulimwacha na matokeo bora mwaka huu huku miezi sita kabla ya kutua Vienna alikuwa ametwaa ushindi katika mbio za London Marathon mara nne kwa mpigo. Eliud Kipchoge aliibuka kuwa chaguo bora na kunyakua taji hilo la BBC, kwa kuwabwaga washindani wenzake akiwemo mwanariadha wa mazoezi ya viungo Simone Biles kutoka Marekani na nahodha wa timu ya taifa ya Raga ya Afrika Kusini Siya Kolisi. Mchezaji Kriketi wa Australia Steve Smith, mchezaji gofu duniani wa Marekani Tiger Woods na mshambuliaji wa Marekani Megan Rapinoe pia waliorodheshwa kuwania tuzo hiyo. Kipchoge aliibuka kuwa bora baada ya kuzoa kura nyingi zilizopigwa kwenye mtandao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako