• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ofisa wa UM aipongeza China kwa kupata mafanikio makubwa katika kulinda usalama wa chakula

  (GMT+08:00) 2019-12-16 10:27:57

  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO Qu Dongyu ameipongeza China kwa kupata mafanikio makubwa katika kulinda usalama wa chakula. Akiongea pembezoni mwa Kongamano la Vijana Duniani linaloendelea mjini Sharm El Sheikh, Misri, Qu amesema China imewapatia chakula asilimia 22 ya watu wa dunia kwa asilimia 7 tu ya ardhi inayofaa kulimwa duniani. Amesema sera nzuri ya kilimo, uvumbuzi na usimamizi mzuri ni muhimu kwa China kufanikiwa kulinda usalama wa chakula. Ameongeza kuwa serikali ya China pia imetekeleza sera tulivu ya kuvutia uwekezaji katika kilimo kutoka sekta ya umma na sekta binafsi na kujenga soko wazi la kuvutia uwekezaji wa kigeni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako